Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka Taasisi zote za Umma ambazo zinadaiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuhakikisha zinalipa madeni yao kabla ya Juni 30, 2017.
Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo, Mjini Dodoma katika viwanja vya Bunge wakati wa uzinduzi wa huduma ya 4G LTE za kampuni hiyo ya simu kwa Mkoa wa Dodoma.
“Kuhusu shilingi Bil. 11.5 ambazo TTCL inazidai Taasisi mbalimbali za Umma, Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, kaa na wadaiwa sugu wote, thibitisheni madeni husika kisha mkubaliane namna ya kulipa madeni hayo. Nijuavyo kila Wizara inatenga bajeti kwa ajili ya ankara za simu, sasa hayo malimbikizo yanatoka wapi?” alisema Kassim Majaliwa.
Aidha amezitaka Taasisi hizo zinazodaiwa na TTCL kuhakikisha zinakamilisha madeni yao kabla ya kufikia Juni 30, 2017 ili kampuni hiyo iweze kufanya kazi ipasavyo na kuendana na ushindani wa kibiashara uliopo.Pia, ameitaka kampuni hiyo kujifunza kutoka kwenye makampuni binafsi namna yanavyoendeshwa na kuiga baadhi ya mbinu zao, hususan katika kupunguza gharama za uendeshaji.
Kassim Majaliwa amesema kwamba, Serikali ina matarajio makubwa kutoka katika kampuni hiyo kutokana na kuwa na imani kwamba kampuni hiyo ina maarifa ya kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa kwenye sekta hiyo.
Vile vile ameitaka kampuni hiyo kujifunza kutoka katika mashirika ya Umma ya Simu kwenye nchi nyingine ambayo yanajiendesha kwa faida, kwa kuiga mbinu ambazo wanazitumia na kuziweka katika muktadha wa nchi ya Tanzania.
Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa pamoja na timu yake kwa hatua ambayo kampuni hiyo imefikia. Aidha amemtaka Waziri huyo kufuatilia kwa karibu kampuni hiyo ili iweze kutoa ushindani wa kutosha kibiashara, ijiendeshe kwa faida, itoe gawiwo stahiki kwa Serikali, ilipe kodi na zaidi ya yote fedha za Umma zilizowekezwa ziweze kutumika vizuri.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai (wapili kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai (wapili kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Zhang Yongquan na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...