WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi wao kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
Amesema  mkakati wa Serikali ni kuimarisha uchumi  hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Brazil, China, Italy, Ufaransa, Jamuhuri ya Kidemkrasi ya Congo (DRC) na Uswisi.

Mabalozi hao ni Balozi Dk. Emmanuel Nchini (Brazil), Balozi Elizabeth Kiondo (Uturuki), Balozi George Madafa (Italy), Balozi James Msekela (Uswisi),Balozi Samuel Shelukindo (Ufaransa), Balozi Paul Mella (DRC), Balozi Mbelwa Kairuki (China).

“Serikali inahitaji watu wa kuja kuwekeza katika viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza nje ya nchi, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha tunapata wawekezaji wenye sifa,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kutumia uwakilishi wao katika nchi hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 .
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017. Kutoka kushoto ni Samwel Shelukindo (Ufaransa), Dkt. James Msekela (Uswisi), Mbelwa Kairuki (China), Paul Mella (DRC), Dkt. Emmanuel Nchimbi (Brazil) George Madafa (Italy) na Elizabeth Kiondo (Uturuki). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...