Waziri
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina kipingamizi na wazo la
kuifanya hospitali ya rufaa ya Haydom kuwa ya kanda kwani hatua hiyo
itaupunguzia mzigo Serikali.
“Serikali
hii ni sikivu, na kuifanya hospitali hii kuwa ya kanda ni kazi ndogo.
Kwa hiyo nitamleta Waziri wa Afya aje awaongoze kusimamia vigezo vya
kuifanya hospitali hii iwe ya kanda,” amesema.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Februari 20, 2017) wakati akizungumza
na mamia ya wakazi wa kata ya Haydom kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa kata.
"Serikali
haina kipingamizi na wazo lenu, cha msingi ni vigezo muhimu vifuatwe.
Kwa hiyo, nitamleta Waziri wa Afya awasaidie kuangalia vigezo,"
amesisitiza.
“Kama
vigezo havipo, tushirikiane kuvikamilisha kwa sababu uwepo wa hospitali
hii kwa hadhi ya kanda kunaisadia Serikali kutokana na nafasi yake
kijiografia,” amesema Waziri Mkuu
“Nia
yetu ni kupunguza gharama kwa mgonjwa anayelazimika kutoka Simiyu hadi
Bugando (Mwanza) au kutoka Arusha hadi Muhimbili (Dar es Salaam). Hapa
ni katikati na nimearifiwa kuwa wagonjwa kutoka mikoa mitano ya Tabora,
Simiyu, Arusha, Singida na Manyara wanafika hapa kupatiwa matibabu,”
amesema.
Amesema
Serikali imepokea maombi kwa ajili ya watumishi wanaotakiwa kwenye
hospitali hiyo na kwamba hivi karibuni itaajiri watumishi kati ya 5,000
hadi 6,000 wa sekta ya afya peke yake. “Tumekwishaanza kuajiri, tumeanza
na sekta ya elimu kwa kuajiri walimu 4,693 ambao wote ni wa fani ya
sayansi. Na sekta inayofuata ni ya afya, kwa hiyo hao watumishi 90
wanaohitajika watapatikana kwenye kundi hilo hilo,” amesema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sanamu ya binadamu wakati alipotembelea moja ya darasa la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Februari 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo Februari 20, 2017.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...