Na Zainul
Mzige.
Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema
kwamba wizara yake itashirikiana na wizara nyingine nchini kuhakikisha kwamba
migogoro ya walimu inamalizwa ili kufanikisha utoaji wa elimu kuwa bora na
jumuishi.
Kauli hiyo
aliitoa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika siku ya pili ya
kuhitimisha kwa mkutano ulioshirikisha nchi 13 za Afrika Mashariki kujadili lengo
la nne la elimu kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs).
Alisema
kwamba migogoro ya walimu inayogusa mishahara, marupurupu pamoja na mazingira
bora ya kazi linagusa pia Wizara za TAMISEMI na UTUMISHI na kusema kwamba wao
kama wasimamizi wa elimu watakachoweza kufanya ni kuzungumza na wenzao
kuhakikisha kwamba migogoro hiyo inafutwa ili utoaji wa elimu uendane na
mipango ya kitaifa na kidunia ya lengo la maendeleo 2030.
Pamoja na
kujibu swali hilo Prof Ndalichako alizungumzia
kwamba walimu walikuwa ni ajenda muhimu
na humo walikubaliana kwamba mwalimu ni kila kitu katika utoaji wa elimu
na kuwa hawawezi kufanikiwa katika elimu bora na jumishi bila kuwa na walimu
wenye umahiri, wanaowezeshwa kufanya hivyo.Kutokana na
ukweli huo wamejipanga kuhakikisha kwamba walimu wanapata mafunzo bora na
kuwakutanisha kubadilishana uzoefu.
Alisema kila
nchi itakuwa na mpango mkakati wake na kuonesha viashiria kwamba vinatekelezwa
kwa namna gani. Mwisho wa siku mwaka 2030 mataifa yote yanapaswa kuhakikisha
kwamba agenda namba 4 ya maendeleo endelevu ya elimu imetekelezwa.
Alisema
katika mkutano huo wa siku mbili wa mawaziri wa elimu ulioandaliwa na UNESCO kwa
kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank wamebainisha
kwamba mikakati ya pamoja ni lazima ichukuliwe ili kufanikisha elimu jumuishi
yenye usawa na ubora kwa watu wote huku ikitoa fursa ya elimu kwa wakati wote.
Alisema
kwamba mkutano ulitambua kwamba elimu haina mwisho, elimu inataka kuwa na mfumo
wa kuwa na maendeleo ya kujifunza kwani mambo hayasimami kutokana na kubadilika
kwa teknolojia, hivyo elimu inayotolewa haina budi kujazia nafasi hiyo kwa
kuwapa uhuru watu kujisogeza zaidi.
Alisema nchi
hizo 13 zimekubaliana kwa pamoja kufikia malengo endelevu 2030 kama yalivyosainiwa
na kila nchi mwaka 2015 kwa kuweka mikakati ili mataifa hayo yaweze kufikia
malengo yanayotakiwa.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akielezea jitihada zitakazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu kuelekea utekelezaji wa SDG4 kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akiendesha mjadala wa kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili wa wadau wa elimu kutoka nchi 13 uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conventional Centre (JNICC) jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige)
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, iliyona makazi yake nchini Marekani akielezea kuhusu mradi wa XPRIZE unahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao ukilenga watoto wa miaka 5-12 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Rasilimali Watu na Tafiti za Kisayansi wa Mauritius, Leela Dookon Luchoomon (kushoto) akieleza mipango ya serikali yake katika kuboresha elimu wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank.
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles akizungumza kwa niaba ya nchi wahisani wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...