Ujumbe
wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL Limited) uliwasili Visiwani Komoro tarehe
5 February, 2017. Ujumbe huo ukiongozwa na Bw. Emmanuel Korosso ulipokelewa na
Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania, Visiwani Komoro. Aidha Mwenyekiti
huyo aliongozana pia na Bw. Ladislaus E. Matindi Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL.
Madhumini ya ziara hiyo ilikuwa ni kuja kuangalia namna gani ATCL inaweza
kutanua wigo wa safari zake Visiwani Komoro. Hii ikiwa ni sehemu ya mkakati wa
shirika hilo kuweza kulidhibiti kikamilifu soko la anga la Visiwa vya Komoro
ambapo kwa sasa Soko hilo limekuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashirika
mengine ya Kimataifa kama vile Ethiopian
Airlines, Air Madagscar, Kenya Airways n.k.
Katika
ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kuongozana na Mhe. Balozi kwenda Kisiwa
cha Anjoun na kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa hicho Mhe. Abdou Salami
Abdou. Ifahamike kwamba Shirika la ndege la ATCL hufanya safari zake mara tatu
kwa wiki Visiwani Komoro ambapo ndege hiyo hutua katika uwanja wa Kimataifa wa
Prince Said Ibrahim Jijini Moroni.
Komoro ni Muungano wa Visiwa Vitatu ambavyo
ni Anjoun, Ngazidja na Moheli. Hata
hivyo imeonekana kuwa abiria wengi wanaosafiri kuja Tanzania kwa ajili ya
shughuli za biashara hutokea Katika Kisiwa cha Anjoun. Imejidhihirisha kuwa abiria kutoka Ksiwa cha Anjoun hupata
usumbufu kwa vile hakuna safari za moja kwa moja kutoka Kisiwa hicho kwenda Dar
es Salaam, hali ambayo imeonekana kuongeza ghara za usafiri kwa abiria hao.
Aidha
katika mazungumzo yao na Gavana wa Kisiwa cha Anjoun ujumbe huo uliwasilisha
maombi ya ATCL kupewa kibali cha kutua Kisiwa cha Anjoun ambapo Gavana huyo
aliridhia maombi hayo na kueleza kufurahishwa kwake na dhamira ya ATCL kufanya
safari zake Kisiwani hapo.
Bw. Ladislaus Matindi akisamilimiana na Gavana wa Anjoun Mhe. Abdou Salam Abdou
Mazungmzo yakiendelea katika ofisi ya Gavana
Mhe Balozi akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Kisiwa
Mhe Balozi akiongoza kikao na wadau wa biashara kutoka Kisiwa cha Anjoun.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...