Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imewafaidisha zaidi ya wakazi elfu kumi na nne waishio katika vijiji vya
Lushoto na Bumbuli kwa kuwapatia mawasiliano ya uhakika kupitia ushirika wao na
mfuko wa Maendeleo wa mawasiliano kwa wote UCSAF yaani Universal Communication
Services Fund.Uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa
Airtel katika kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga, umekuja ikiwa ni
wiki moja toka Mfuko wa maendeleo wa Mawasiliano kwa wote na Airtel
walipozindua minara mingine mitatu mkoani Dodoma.
Meneja Mauzo wa Airtel Tanga John Nada alisema "Airtel
tumejipanga kuendelea kutoa mawasiliano ya uhakika hasa kwa kipindi hiki
ambacho TCRA wamezindua huduma ya kuwawezesha wateja kuhama mtandano akiwa
na namba ileile ikiwa hawapati huduma nzuri na za uhakika, hivyo basi kwa
wakazi wa Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga,
Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na
Sakarre Airtel ndio mtandao wenu wa ukahika kwa sasa”
“Tunawaomba wakazi wote mtumie fursa hii
ya mawasiliano kwa kuwa wabunifu zaidi, tumumieni huduma
ya Airtel Money kwa kuwa pia mko mbali na huduma za kibenki tumeni na kupokea
pesa ili kuboreshe kilimo kwa kutumia mawasiliano haya ya uhakika toka Airtel”
alisisitiza Bw, Nada
Kauli ya wananchi juu ya
tatizo la mawasiliano zilithibitishwa na diwani wa kata hiyo ,Mh Edwin Mahunda
kwamba wakazi wa Kata hiyo walikuwa wakipanda juu ya miti na kwenye
vilele vya milima wakitafuta mawasiliano ili kufanya mawasiliano ya kibiashara
na mambo mengine ya kijamii.
“Tunawashukuru sana Airtel na UCSAF kwa
jitihada zao za kutuletea mawasiliano, mawasiliano haya yatasaidia wakazi wa
hapa kijijini na pia yatawasaidia wanaishio mbali na hapa ili kuweza kufanya
shughuli zao vyema, awali hali ilikuwa mbaya sana, ilikuwa huwezi kupiga simu
mpaka ufike sehemu yenye muinuko” alieleza Mh Mahunda-Diwani.
Diwani wa kata ya kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo wa Airtel Tanga John Nada wakikata autepe kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
Vifijo baada ya uzinduzi wa mnara huo
Diwani wa kata ya kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda akiongea na wananchi waliojawa na furaha baada ya uzinduzi wa mnara huo.
Mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
Diwani wa kata ya kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo wa Airtel Tanga John Nada wakiwa katika picha ya pamoja na baasdhi ya wananchi baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...