Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Ubalozi wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Shule za Msingi zilizopata visima hivyo ni Yombo, Umoja , Mwale pamoja na Bwawani. Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait , Jasem Al-Najem amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maji ndiyo maana wameona umuhimu wa visima hivyo katika shule hizo.
Amesema wataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na mahitaji yaliyopo katika jamii kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.
Al-Najem amesema kuwa wameweza kuchimba visima 16 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 63,000 na watu wengine waweze kujitokeza kusaidia jitihada mbalimbali.
Ubalozi huo pia umekabidhi dawa za binadamu katika Hospitali ya Amana zenye thamani sh.milioni tatu.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizundua kisima cha maji safi katika shule ya Msingi Yombo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Ilala , Hamisi Mlangala akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa visima ambapo alishukuru msaada huo.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi dawa kwa Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni, jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akitembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...