MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ameendelea kutatua changamoto mbalimbali za jimbo hilo kwa kufanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi zilizopo katika mjini wa mafinga na kukagua baadhi ya miundombinu inayoendelea kukarabatiwa kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Katika ziara hiyo Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo wawili ya shule, mifuko 10 ya saruji, madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo ambayo yalitolewa na wakala wa shamba la miti Sao Hill huku chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mafinga Mji kupitia mwenyekiti wake Yohanes Cosmas wakichangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mbunge za kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo.

Katika hatua nyingine mbunge huyo alitembelea jengo jipya la ukumbi wa kisasa lililojengwa na kikundi cha Agape group ambalo lipo kwenye kata ya Kinyanambo kwa lengo la kuinua kipato cha halmashauri hiyo.
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi madawti kwa viongozi wa kata ya sao hill kwa ajili ya matumizi ya shule.

imeandikwa na Fredy Mgunda,Mafinga.
 
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipongezwa na viongozi wa kata ya sao hill kwa jitihada wanazozifanya kuleta maendeleo katika jimbo la mafinga mjini.
Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo ya shule hii.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...