Matunzo ya mtoto
hasa kwa wazazi
waliotengana ni pamoja na
chakula, makazi, mavazi,
elimu, pamoja na
malezi bora. Wazazi wote
kwa pamoja yaani
baba na mama
wanao wajibu kila mmoja
kwa nafasi yake kuchangia katika
matunzo ya mtoto.
Aidha makala haya
kupitia Sheria ya Mtoto ,Na. 21
ya 2009 yatajibu
ikiwa suala kutoa
matunzo ya mtoto
ni la milele
au linao muda
maalum. Lakini kabla ya
hayo tutizame nani
ana mamlaka ya kufungua
shauri kudai matunzo
ya mtoto.
1. NANI ANAWEZA
KUFUNGUA SHAURI LA
MATUNZO.
Wengi wetu twajua
kuwa ni mama wa
mtoto pekee ndiye
anayeweza kufungua shauri la
mtoto kupatiwa matunzo.
Dhana hii si
kweli.
Kifungu cha 42( 1 )
cha Sheria ya
Mtoto kinawataja wafuatao
kuwa na mamlaka
ya kuomba mtoto apatiwe
matunzo :
( a ) Mzazi wa
mtoto. Kifungu hakikutaja
mama wa mtoto bali
mzazi wa mtoto. Kwahiyo hata
baba anaweza kufungua
shauri akimtaka mama
kutoa matunzo ya
mtoto. Mama kumtelekeza
mwanae nako ni kumnyima mtoto
matunzo .
Wako mama wanakimbia
nyumba zao na
kuwaacha watoto. Unaweza kutumia
kifungu hiki kumtaka
mama amchukue mwanae na
akae nae ikiwa
ni sehemu ya
matunzo.
( b ) Mlezi wa mtoto
naye amepewa mamlaka
ya kufungua shauri
kuomba matunzo ya
mtoto. Wako watu
wako mjini lakini
wamewaacha watoto vijijni
wakilelewa na ndugu au
rafiki.
Lakini pia yapo
mazingira ambapo kwa
amri ya mahakama
imeamriwa mtoto asikae
na wazazi bali
akae na mlezi
kutokana na sababu mbalimbali. Au kwasababu
nyingine yoyote mtoto anakaa
na mlezi .
Basi ni katika
hali hiyo mlezi
huyo anayo mamlaka
ya kuomba au
kufungua shauri akishinikiza
mzazi/wazazi kutoa matunzo
ya mtoto.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...