Katibu
wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile
akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jumuia hiyo kutoka katika Kata
mbalimbali za wilaya ya Ilala, alipokutana nao katika kikao maalum cha
kujitambulisha kwao, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM wilaya
ya Ilala. Kulia ni Katibu wa Jumuia hiyo wilaya ya Ilala, Lugano
Mwafongo.
Akizungumza
kwenye kikao hicho, pamoja na mambo mbalimbali Mkandawile ameitaka
Jumuia ya Wazazi katika mkoa wake na maeneo mengine nchini, kuunga mkono
hatua ya serikali kuingia katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Mkandawile
amesema, Kama sehemu ya Wanana CCM, Jumuia hiyo haiba budi kuunga mkono
mabambano hayo kwa kuwa Serikali inatekeleza ilani ya CCM, ibaraya 118
hadi 119.
Katibu
wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akiwasili
ukumbini. Kushoto ni Katibu wa Jumuia hiyo wilaya ya Ilala, Lugano
Mwafongo na kulia ni Katibu wa Jimbo la Ilala Christopher Lugemalila.
Wajumbe
wakimsikiliza Mkandawile wakati akizungumza na watendaji na viongozi wa
Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Ilala. Picha zote na Bashir Nkoromo.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...