Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba,  akitoa ufafanuzi  kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara yake kwa Bajeti ya mwaka wa fedha wa  uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 
 Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Balozi  Hassan Simba Yahaya anayemfuatia wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini [IGP] Ernest  Mangu aliyesimama  kuhusu Oparesheni mbalimbali za kuzuia uhalifu hapa nchini, wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala, akiwa pamoja na watendaji wengine wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, akimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Balozi  Adad Rajab wakati Mwenyekiti huyo hayupo pichani, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kuipitia Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bjeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.   
 Katibu Mkuu wa Wizara Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wake, Balozi  Hassan Simba Yahaya wakifuatilia kwa makini Bajeti ya Jeshi la Polisi ya mwaka ujao wa fedha,  katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ambapo kwa siku ya leo Kamati hiyo imepitisha Bajeti za Jeshi la Polisi na Fungu Hamsini na Moja inayobeba Idara Saidizi ndani ya wizara, hatua ambayo ni muhimu kufikiwa kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba,  akisoma taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa  uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kabla ya Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma  mkoani Dodoma.
PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YANCHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...