Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Sampuli ya Mchanga wenye Dhahabu unao safirishwa Nnje ya Nchi na Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama Mkoani Shinyanga Waziri Mkuu Alifika katika Mgodi huo 27march2017 kuangalia na kuchukua Sampuli ya Mchanga ili Serekali Ikaupime katika Maabara za Serekali.
Mtaalamu wa Madini akiweka Sampuli ya Mchanga katika Mfuko kutoka katika baadhi ya Makontena na kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nakuondoka nao kwa ajili ya kuupeleka katika Maabara ya Serekali inayo shugulika na Upimaji wa Madini Wziri Mkuu alifanya ziara katika mgodi wa Buzwagi 27March2017 kwalengo ya kujionea aina ya Mchanga unao safirishwa nnje ya Nnchi na Baadhi ya Migodi inayo Chimba Dhahabu hapa Nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa afanya ziara katika Mgodi wa Buzwagi 27 March 2017 kwa ajili ya kuangalia Mchanga uliowekwa katika Makontena kwa ajili yakusafirishwa nnje ya nchi katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Bwana Stewart Hamilton.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi
uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga
katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu
wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema
wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani
cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni
sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa
tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.
Waziri
Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na
kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya
kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena
yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua
kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaji anasema wanaupeleka nje ya
nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata
hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu
kifanyike hapahapa,”
Waziri
Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo
nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka
kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama
yanastahili.
Aliongeza
kwamba “Hili lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya
madini nchini kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza
fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Wakati
huohuo Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuwa nasubira wakati Serikali
ikiendelea na zoezi la kuchunguza athari zitokanazo na kusafirisha
mchanga wa madini nje ya nchi. Pia amewatoa wasiwasi wafanyakazi katika
migodi na wamiliki kutowapunguza na badala yake waache waendelee na
majukumu yao.
Kwa
upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema
mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na
vibarua 500.
Alisema
kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila
kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za
madini ya shaba.
Bw.
Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia
50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya
shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya
kutenganishwa.
“Hapa
Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam
kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku
tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu
zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam
Cargo Dar es Salaam,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...