Katika mpango wa kuboresha
makazi yaliyojengwa kiholela, Kimara imekuwa mojawapo wa maeneo yanayoendelea
na zoezi la Urasimishaji. Kwa sasa hatua iliyofikiwa ni ya uwekaji wa barabara
za mitaa.
Halmashauri
nyingine 6 zilizopangwa kutekeleza mradi huu ni; Manispaa za Musoma,
Kigoma-Ujiji, Tabora, Singida, Sumbawanga na Lindi ambapo viwanja 3000
vitapimwa katika kila Halmashauri.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi inatekeleza mradi wa
kurasimisha maeneo yaliyojengwa kiholela katika Jiji la Dar es Salaam katika
kata ya Kimara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Ubungo. Jumla ya viwanja
6,000 vinatarajiwa kupimwa na kumilikishwa. Katika mitaa ya Makongo juu, na
Chasimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo jumla ya viwanja
6585 vitapimwa.
Urasimishaji utaongeza
huduma za jamii na miundombinu katika makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa
kutoa hati za kumiliki ardhi kwa muda mrefu. Mpango huu unatekelezwa kwa
kushirikisha wananchi na viongozi wa maeneo husika.
Katika mpango huu, Wananchi
wanawajibika kuonyesha mipaka ya miliki zao pamoja na kuchangia ardhi kwa ajili
ya barabara. Aidha kila mwananchi anawajibika kutoa taarifa kwa usahihi ili
kurahisisha umilikishaji. Urasimishaji unatekelezwa kulingana na sheria ya
Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999 fungu la 56-60
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi inawasihi Wananchi kushirikiana vyema katika zoezi hili kote nchini
ili kuepuka Makazi holela kwa Maendeleo
ya Taifa.
Vile
vile, Wizara itaendelea kushirikiana na Halmashauri nchini kuandaa mipango ya
zoezi la Uramishaji. Baada ya Urasimishaji; miji inatarajiwa kuendelezwa kwa
kulingana na mapendekezo ya mipango kabambe.
Mjumbe katika kamati ya
Mipango Miji – Chasimba; Bi Hawa Haruna Kimaro akitoa maelezo kwa Wananchi
kuhusu zoezi la upimaji linavyoendelea
Chasimba.
Zoezi la Urasimishaji
linavyoendelea Kimara, ambapo zoezi hilo lipo kwenye hatua ya uwekwaji wa
barabara za mitaa.
Afisa Mipango Miji, akiwa
katika zoezi la upimaji Chasimba.
Dhana ya ushirikishwaji wa
Wananchi inavyotekelezwa katika zoezi la Urasimishaji; Wananchi
wakieleweshwa na wapima jinsi upimaji unavyofanyika katika eneo la
Chasimba
Wananchi wakishuhudia uwekaji
wa Barabara katika mitaa yao – Kimara.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...