Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli
ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika Elimu Kibaha
Dkt. Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za
kiutendaji zinazomkabili.
Akijibu swali la Waandishi wa Habari waliotaka kupata ufafanuzi juu ya
hatma ya tuhuma mbalimbali zinazolikabili Shirika la Elimu Kibaha ambazo
zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa,
Mhe. Simbachawene alisema kutokana na kuwepo kwa tuhuma mbalimbali
za uendeshaji, Mhe. Rais Magufuli tarehe 4/3/2017 ametengua rasmi
nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi.
“ Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha
likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo
kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka
kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya
uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa
hoja zinazohitaji uchunguzi zaidi. Hivyo, ili uchunguzi huo uweze
kufanyika Mhe. Rais amemsimamisha kazi Mtendaji huyu Mkuu wa
Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake.
Alisema Mhe. Simbachawene
Alisema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwakuwa tuhuma za
awali zilizojitokeza dhidi yake zinajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa
uchunguzi zaidi.
Kwasasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa
hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...