Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika ziara ya kukagua sehemu zilizokumbwa na mafuriko katika bonde la Mto Msimbazi, baada ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Na Ripota wa globu ya jamii

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.

Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa akitembelea maeneo hayo.

"kulingana na utabiri wa hali ya hewa mvua hizi zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50, maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba "Amesema Makonda

amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia ili kuweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi ili kupunguza Madhara, kwani yanayo onekana leo ni tabia mbaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunapoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi, pia tunaambiwa tuhakikishe kuwa hatuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika moja ya nyumba zilizopo kando ya bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na adha ya mafuriko yaliyotokana na mvua ilinyosha jana.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mto Msimbazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...