Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI)
umezindua mfumo maalum wa kuuza,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu
iitwayo “UWARIDI APP” leo Jijini Dar es Salaam.
Akizindua Programu hiyo Katibu Mkuu wa Umoja huo
Bw. Bw.Ibrahim Gama amesema kuwa wameamua kuanzisha programu hii ili
kuwawezesha wanachama wa UWARIDI kuweka riwaya zao kwa ajili ya kuuzwa na wao
kujipatia malipo kutoka kwa mtengenezaji wa app hiyo.
“Kwa miaka mingi waandishi wa riwaya wamekuwa
wakijaribu kutafuta njia mbalimbali za kunadi kazi zao ili kuwafikia wasomaji
wao kwa urahisi,na tukaona changamoto wanazopata katika kuzipata kazi zetu na
hivyo tukaamua kuandaa program hii itakayowawezesha kupata riwaya zetu kwa
urahisi zaidi kwani utahitaji kuwa na programu hii tu kwenye simu yako ili
kusoma muda wowote”,Aliongeza Bw.Gama.
Katika mfumo huo kutapatikana riwaya za waandishi
mchanganyiko ikijumuisha waandishi nguli na wachanga ambapo mpaka sasa zaidi ya waandishi 20
wameweka riwaya zao katika mfumo huo na zinaendelea kuongezeka kila siku.
Katibu wa Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) Bw.Ibrahim Gama akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa programu(App) ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” iliyozinduliwa na Umoja huo leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Rais wa UWARIDI Bw.Hussein Tuwa.
Rais wa Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) Bw.Hussein Tuwa akizungumzia uanzishwaji wa programu(App) ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” iliyozinduliwa na Umoja huo leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu wa Umoja wa umoja huo Bw.Ibrahim Gama na Abdillahi Muna kutoka Dau Technology ltd.
Mwakilishi kutoka Dau Technology Limited Bw.Abdillahi Muna(wa kwanza kulia) akieleza jinsi program ya “UWARIDI APP” iliyozinduliwa leo na Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) kwa ajili ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu.Dau Technology ndio watengenezaji wa App hiyo.Wengine ni Rais wa Umoja huo Bw.Hussein Tuwa na katibu wake Bw.Ibrahim Gama.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...