Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Ashaji amesema kwamba
Mfumo jumuishi wa kifedha ni muhimu katika kujenga uchumi wa Taifa la
Tanzania.
Dkt.Kijaji
ameyasema hayo jana wakati wa mkutano wa tatu wa Kitaifa juu ya huduma
rasmi za kifedha kwa vikundi vya hisa na mjadala wa masuala ya kisera na
Sheria katika uhusishwaji wa kifedha.
Alisema
kuwa ili kuhakikisha swala hili linafanyiwa kazi, Serikali imeandaa
sera ya mwaka 2006 inayohakikisha mifumo isiyo rasmi ya kifedha inakuwa
rasmi na watu wote wanakuwa wamejumuishwa katika mfumo sahihi wa
matumizi ndani ya sekta ya kifedha.
Dkt. Kijaju alisema kuwa moja ya changamoto katika mfumo usio rasmi wa kifedha ni kukopeshwa kwa riba kubwa na watu wanaofanyakazi katika mifumo hiyo, lakini hawajarasmishwa rasmi,hali inayouwaumiza Wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla.Dkt Kijaji akaongeza kuwa kutokana namfumo huo, Serikali sasa inaandaa sheria kwa ajili ya huduma ndogo za kifedha ilikuwekea mazingira rafiki ya kufanya kazi zao.
Pia aliongeza kuwa Care international amekuwa mdau mkubwa katika maendeleo ya uchumi nchini Tanzania, sio kifedha tu lakini pia sekta ya afya,Kilimo na maeneo mbalimbali,hivyo aliwasihi wananchi waendelee kuwapa ushirikiano ili kuleta maendeleo zaidi nchini.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia Care International Nchini Tanzania Bw. Paul Daniel alisema kuwa lengo la mkutano huo ni muendelezo wa utamaduni wa Care kutoa Fulsa ya kupeana taarifa kwa wadau walio ndani ya sekta hiyo,lengo kubwa ni kuongeza umoja na ushirikiano katika kuhamasisha uhusishwaji wa kifedha katika vikundi vya hisa.
Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wa Serikali wakiwemo Wizara ya Fedha na Mipango,Benki kuu ya Tanzania,TAMISEMI na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) pia Taasisi za kifedha na Sekta mbalimbali,ikiwa ni juhudi za Care nchini Tanzania ambazo zimelenga katika kutoa Fursa kwa jamii kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa ubia wakiwahusisha sekta binafsi, Serikali,wabia wa maendeleo na asasi za Kiraia (CSO's) .Mkutano huo uliandaliwa na Asasi ya kiraia ya Care International ya Nchini Tanzania.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza na wadau
mbalimbali wa sekta za Serikali na Sekta binafsi katika hafla hiyo
iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wadau waliohudhuria katika mkutano huo.
Mmiliki wa Vikundi vya Kifedha (VIKOBA) Mwalim Monica akitoa ufafanuzi zaidi namna gani alivofaidika kupitia Care International pamoja na taasisi za kifedha. Picha na Yasir Adam Globu ya Jamii
Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia wa Care International Nchini Tanzania Ndugu Paul Daniel akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mbele ya Wadau,huku akielezea kwa ufupi lengo la na Mafanikio ya Care International
Mkurugenzi
Muendeshaji wa Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Fedha (FSDT) Bi,Irene
Mlola akizungumza namna walivyo panua wigo na mafanikio yao katika
vikundi mbalimbali vyenye uhitaji wa kifedha nchini Tanzania
Baadhi ya Wadau waliohudhuria katika mkutano huo
Mkurugenzi
wa Masoko na Maendeleo ya Biashara Bw. Deo Kwiyakwa akizungumza kuhusu
Sera,sheria zinavyokwamisha Maendeleo katiaka Taasisi za Kifedha
Mkurugenzi wa Programu (GEWE) Bi Mwanahamisi Singano akizungumza jambo katika Mkutano huo ulio wakutanisha Sekta za kiserikali na sekta binafsi










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...