Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- leo imeungana na wanawake
wengine ulimwenguni kote kuadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.

Zoezi hilo limeongozwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Dar
es salaam Mheshimiwa Angellah Kairuki kwa niaba ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi –UWT- mkoani humo.

Mheshimiwa Kairuki ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora amesema katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani UWT imeona ni vema wakashiriki
katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuonesha dhamira ya dhati kwamba CCM inawajali wananchi wake bila kujali itikadi ya chama.

‘’ Sisi tumekuja hapa Muhimbili kushiriki na nyinyi katika kuadhimisha
siku hii kwa kufanya usafi bila kujali itikadi ya chama kwani Hospitali hii
inahudumiwa wananchi wote , pia siku hii ya leo tunatoa msaada wa vifaa mbalimbali vya watoto na wenzetu wengine wameenda katika Hospitali
zingine wote tukiwa na lengo moja’’. Amesema Waziri Kairuki.
Waziri Kairuki (wa pili kutoka kushoto) akifanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Muhimbili, Agness
Mtawa. Kutoka kulia wa kwanza ni Katibu wa Umoja wa Wanawake katika Wilaya ya Ilala, Joyce Ibrahimu Mkaugala na Zuhura Mawona wakifanya usafi Leo katika hospitali hiyo.
Waziri Kairuki akizungumza na kinamama waliojifungua watoto kabla ya kuwapatia zawadi ya nguo za watoto, pampazi na sabuni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki akizungumza na  wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo kabla ya kukabidhi vitanda 10 na magodoro 10 kwa uongozi wa hospitali hiyo. Katika kusherekea siku ya wanawake duniani leo, pia Waziri huyo amewapatia kinamama zawadi mbalimbali zikiwamo nguo za watoto na sabuni. Kushuto Mkurugenzi wa Uunguzi katika hospitali hiyo, Agness Mtawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...