Asasi ya Kibunge inayojihusisha na masuala  ya Idadi ya watu na maendeleo (TPAPD) imeelezea umuhimu wa kuweka kipaumbele kwenye masuala ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la kasi la idadi ya watu  ambayo kwa sasa ni wa asilimia 2.7 kwa mwaka.

Tamko la TPAPD lilitolewa leo katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, limesema matumizi ya njia za uzazi wa mpango yanaweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi (MMR) kwa asilimia 44, na kupunguza vifo vya watoto kwa asilimia 35. Vifo vya wanawake katika uzazi vimefikia 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2015 kutoka vifo 454 katika kila vizazi hai mwaka 2010.

TPAPD chini ya Mwenyekiti wake Mhe Dkt Mary Mwanjelwa iliamua kutoa tamko hili hivi karibuni katika kikao cha kamati tendaji mjini Dar es Salaam kilichojadili umuhimu wa uzazi wa mpango katika harakati za kujenga Tanzania ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda.

Tamko hilo lililotiwa saini na Mwenyekiti Dkt Mwanjelwa limesema:
“uzazi wa mpango unahitajika katika kuiwezesha nchi kukabiliana na ongezeko la kasi la idadi ya watu inayochangiwa na uzazi wa kiwango cha wastani wa watoto sita kwa kila mwanamke aliye katika umri wa uzazi. Hali hii huchangia utegemezi pamoja na umaskini; na pia hudumaza juhudi za taifa za kufikia malengo ya maendeleo”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...