Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA) imeanzisha mfumo wa Tehama unaowawezesha wanachama kufuatilia malalamiko yao na kuwezesha SSRA kuyashughulikia kwa urahisi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Afisa Mwandamizi TEHAMA wa Mamlaka hiyo, David Nghandi amesema mfumo huo unaotambuliwa kwa jina la SSRA kutuma malalamiko yao na kuiwezesha mamlaka hiyo kuyashughulikia.
"Mfumo huu unapatikana kwa njia ya mobile application (App) unapatikana kwa watumiaji wa simu za mkononi za android kupitia google play"alisema David.
Afisa huyo ameongeza kuwa mfumo huo umeweka utaratibu kwa mlalamikaji kufuatilia hatua za utatuzi wa malalamiko yake kwa kutumia kumbukumbu za mlalamikaji.
"Mfumo huu wa malalamiko umezingatia uhifadhi wa kumbukumbu kwa upande wa mamlaka na kurahisisha ufuatiliaji wa malalamiko pamoja na kutoa mrejesho kwa haraka bila kujali mahali alipo na utasaidia kupunguza gharama za kufuatilia malalamiko yake"aliongeza Afisa huyo.
Mamlaka inatoa wito kwa wanachama na wananchi wote kwa ujumla kutumia mfumo huu kwa sababu unarahisisha mawasiliano kati ya mlalamikaji na mamlaka hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA), Sarah Kibonde akitoa Ufafanuzi kuhusiana na Mfumo huo wa kutuma malalamiko kwa njia ya Simu. Wengine pichani ni Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Ernest Masaka na katikati ni Afisa Mwandamizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), David Nghambi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...