Family ya Frederick Malika ya Kijitonyama Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Mr. Raphael Frederick Malika kilichotokea Jumanne Tarehe 14 March 2017 hospitali ya Muhimbili. Habari ziwafike ndugu, jamaa na marafiki popote walipo.
RATIBA YA MAZISHI:
Jumamosi, 18 March 2017
• Saa 7 Mchana – Misa Takatifu - St Albans Church, Dar es salaam City Center
• Saa 8 Mchana - Heshima za mwisho kwa Marehemu - St Albans Church, Dar es salaam City Center
• Saa 9 mpaka Saa 10 Mchana - Safari ya kuelekea Makaburi ya Kinondoni - Shughuli za Mazishi kwenye Makaburi ya Kinondoni (Ndani)
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
jina la Bwana lihimidiwe.
AMEN!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...