Na Woinde Shizza,Arusha
Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure
zoezi hilo ambalo limeanza jana jijini hapa, katika uwanja wa sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi,kwani zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao bure katika viwanja hivyo
Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maadhimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha,Mkurugenzi wa Phide Entertaiment,Phidesia Mwakitalima alisema kuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi .
Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao hivyo ni jambo zuri mno
Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa, kitu ambacho sio kizuri na amewataka wananchi kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara
Zoezi hili la kupima afya limeanza jana na linatarajiwa kumalizika Machi 8,mwaka huu na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake .

Baadhi ya wananchi wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka KCMC pamoja na Mounti meru Hospital, ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide Entertaiment

Baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa ,Ukimwi na mengineyo

Mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani viwanja vya Sheikh Amri Abeid
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...