Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na ujio wa mmoja wa Wasanii mahiri katika tasnia ya Filamu nchini Nigeria,Mike Ezuronye nchini Tanzania,ambaye amewasili nchini kwa mradi maalumu wa kutengeneza filamu.Waziri Nape amesema kuwa ujio wa msanii huyo ni hatua kubwa katika Tasnia ta filamu nchini,kwani ujio wake utaongeza chachu ya mabadiliko kwa namna moja ama nyingine kwa wasanii wenyewe na sanaa yenyewe kwa ujumla.
"Huyu ni mmoja wa wageni waliokuja na wengine wataendelea kuja,Sisi kama Serikali kazi yetu ni kunatengeneza mazingira mazuri waje zaidi katika nchi yetu,waje washirikiane na sisi,Wakija wataleta teknolojia,wataleta ujuzi na uzoefu wao lakini pia wakishirikiana na wasanii wetu kufanya kazi zao,kazi zetu zitaingia kwenye nchi yao na za kwao zitaingia kwenye nchi yetu na sote kwa pamoja tutafaidika kama nchi na wasanii kwa ujumla,
.
Amesema kuwa imefika wakati wasanii wa Tanzania waone haja ya kutumia sanaa zetu za Filamu na muziki kuliunganisha bara letu la Afrika,amesema kuwa hilo ni jambo kubwa sana na anatamani Watanzania na wasanii wenyewe kwa ujumla waone wajibu walionao katika kuzitumia kazi zao kulifanya bara la Afrika kujivunia kazi za wasanii wake popote pale ulimwenguni.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Entertaiment Project and Design (EPD) Halima Yahaya
almaarufu kwa jina la kisanii Davina akizungumza na Waandishi wa habari
mapema leo jijini Dar,kuhusiana na ujio wa Msanii Nguli wa Filamu kutoka
nchini Nigeria,Mike Ezuronye nchini Tanzania.
Davina amesema kuwa ujio
wa msanii huyo umefanyika kwa Msaada mkubwa wa Serikali kupitia Wizara ya
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo.Anasema wamefanikiwa kumleta msaniii huyo
kupitia kampuni yake kwa ajili ya kufanya mradi (Project) ya Filamu hapa
nchini,Davina amesema kuwa msanii huyo mahiri anatarajia kukaa nchini
kwa wiki mbili mpaka pale mradi huo utakapokamilika.Pichani kulia ni
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye.
Msanii Nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria,Mike Ezuronye akizungumzia ujio wake hapa nchini,kwa Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,Pichani kulia ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Msanii huyo wa nyota wa Filamu kutoka nchini Nigeria,alipokuwa akizungumzia ujio wake hapa nchini.Picha na Michuzi Jr.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...