Serikali imewataka viongozi wa kisiasa pamoja na watendaji wa
serikali kutotumia madaraka yao vibaya kuwanyanyasa na kuwasumbua
wawekezaji wazawa waliowekeza ndani ya nchi.
Aidha
viongozi hao wametakiwa kuwaheshimu na kuwajengea mazingira rafiki
yatakayowawezesha kufanya biashara zao kwa amani ili kuweza kukuza
uchumi wa taifa na kuongeza ajira kwa vijana. Kauli hiyo imetolewa jana
na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda mkoani Simiyu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa
uwekezaji wa mkoa huo pamoja na tovuti ya Mkoa.
Prof.
Mkenda amewasihi viongozi wote wa serikali ngazi za mikoa na wilaya
nchini kujivunia uwepo wa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ambao
ni wazawa kwani wao ni chachu ya kuongeza kwa ajira za vijana.
Amesema kuwa si vyema wafanyabishara kutukanwa, kutolewa lugha
zisizokuwa sahihi na kuonekana kama wana uadui na serikali, na badala
yake watukuzwe ili kuweza kulipa kodi pamoja na kufuata sheria na
taratibu za nchi.
“hawa wafanyabishara hasa wazawa na
wajasiriamali tuwaone kama wenzetu, ndugu zetu na watu muhimu, kwani
wameajiri vijana wetu, wanalipa kodi ili nchi ipate maendeleo, lakini
wanatekeleza kauli mbiu ya Rais, Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
tuwathamni” alisema Prof.Mkenda. Katibu Mkuu huyo amezitaka halmashauri
zote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji wakubwa
na wadogo kwa ajili ya kujenga viwanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...