MWENYEKITI
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni
wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini.
Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika hoteli ya
Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa 50 ya Ufaransa
wakiongozwa na Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku
wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro.
Akizungumza
kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi
alisema katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha
shukurani kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza.
Alisema jioni hii ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya
kuwakarimu wageni hao ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya
uchumi na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati)
akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa
katika hafla maalum ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya
ugeni huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia
leo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)
“Ujio
wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia
hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa
ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili.
Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa
kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki
mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia.
Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa
sasa utaendelezwa zaidi.
Aliwatakia wageni wake chakula chema..
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha
wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni
aliyoiandaa maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena
jijini Dae es Salaam.
Mgeni
rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema
kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye
anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano.
“ …Business and friendship goes Together..” alisema balozi huyo kwa
lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana na chakula hicho
anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si wa
kubahatisha unakua.
Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus,
Siemens, General electrical na kadhalika.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi
wa Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni
mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa
wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la
ukaribisho kwenye 'cocktail' kabla ya kushiriki chakula cha jioni na
wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...