Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa katika dimba la Kaitaba, Mjini Bukoba Mkoani Kagera.
katika mchezo huo ulishuhudia timu ya soka ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph na bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la kufutia machozi kwa Simba likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi cha pili.
Kwa matokoe hayo Yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 56 wakifuatiw na Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na Azam wenye pointi 44.
Kikosi cha Simba kilichoanza.
Kichuya Akiambaa na Mpira.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...