Mratibu
wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi
shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw.
Elinasi Monga akifundisha somo la mabadiliko ya tabia nchi ambalo
aliweza kukazia suala la waandishi wa habari kujua visababishi na
viashiria ambavyo ni vyema kujua na kuweza kuvifanyia kazi kwa ufasaha
zaidi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Picha
zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.
Katika mafunzo hayo Mratibu wa Mradi huo alisema kuwa wakulima wadogo
wadogo ndiyo wanaathika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa
wamekuwa hawana uelewa mzuri katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aliongeza jambo lingine linalorudisha nyuma ni serikali za mitaa kukosa
mipango mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwisho alisisitiza uongozi mbovu katika sekta ya misitu huchangia
uharibifu wa misitu kwa kiasi kikubwa.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Elinasi Monga akisisitiza jambo.
Mratibu
wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akifundisha somo juu ya kiwango
vya athari ya mabadiliko ya tabia nchi, Nyenzo shirikishi pamoja na
umuhimu wa misitu ya jamii ambavyo ni muhimu kwa waandishi wa habari
kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017
mjini Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...