BENKI ya NMB imekutanisha wafanyabiashara zaidi ya
500 wa jijini Dar es Salaam waliopo katika jumuia ya wafanyabiashara wa
NMB "NMB Business Club" kwa lengo la kutoa mafunzo mbalimbali ya
biashara pamoja na mafunzo ya kodi ili kukuza biashara zao.
Kundi
hilo la NMB Business Club mkoa wa Dar es Salaam limekutanishwa kwa
pamoja ili wafanyabiashara hao waweze kujuana na kubadilishana uzoefu
katika shughuli zao jambo ambalo litachangia wao kushikamana na
kunufaika zaidi na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Akizungumza
na wafanyabiashara katika mkutano huo, Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha
Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela alisema katika semina hiyo
wataalam wa biashara wa Benki ya NMB watatoa mafunzo mbalimbali ya namna
ya kukuza biashara na kuelezea fursa anuai zilizopo ndani ya benki hiyo
ili wateja wao waendelee kunufaika nazo. Alisema mbali ya kutoa mafunzo
ya biashara na kodi wana NMB Business Club walioshiriki katika mkutano
huo watapata fursa ya kutoa mrejesho dhidi ya huduma wanazopewa ili
benki iangalie namna ya kuzishughulikia.
Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...