Na Mathias Canal, Dar es salaam.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo kwa kauli moja limeridhia na kuagiza
Idara ya Mipangomiji na Mazingira kufuatilia na kutwaa maeneo kwa ajili ya
matumizi ya Umma hususani maeneo ya Shule.
Aidha Baraza la madiwani limeagiza Idara hiyo ya Mipango Miji kutembelea na
kupima eneo la shule ya Sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba ambalo eneo lake
limesalia ekari 31 kati ya 22 huku eneo jingine likitumiwa na wananchi kinyume
na utaratibu.
Pia imebainika kuwa hali ya ukusanyaji mapato inaendelea kukua kutokana na
juhudi na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato tangu kuanza
kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo baada ya mgawanyo wa Halmashauri hiyo
kutoka Manispaa Mama ya kinondoni.
Akijibu swali lililoulizwa kuhusu ubovu wa mashine za
kukusanyia mapato POS Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema
kuwa hajawahi kupokea malalamiko juu ya mashine hizo na kubainisha kuwa
Manispaa imepata mtaalamu anayeshughulikia mashine hizo ambapo atatoa taarifa
juu ya kiasi kilichokusanywa tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo za POS.
Akiongelea kuhusu semina kwa madiwani MD Kayombo alikiri
kuwa kuna umuhimu wa madiwani kupata semina hususani kwenye eneo la kanuni na
sheria mbalimbali na pia katika sheria za manunuzi hivyo ameahidi kuandaa
semina hiyo ili waweze kuelimika zaidi.
MD Kayombo akizungumzia suala la maendeleo ya jumla katika kuboresha miundo
mbinu katika shule za Manispaa ya Ubungo alisema kuwa zitakuwa zikifanyika
hatua kwa hatua katika kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa huku akibainisha
kuwa katika kuinua elimu katika Shule za Manispaa ya Ubungo ujenzi wa Madarasa,
Vyoo sambamba na Ukuta vitaanza kujengwa hivi karibuni katika shule ya Msingi
Ubungo Plaza.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakiwa kwenye Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Waheshimiwa Madiwani wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakisoma muongozo wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...