Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewasili mjini Arusha jioni hii ambapo hapo kesho ataongoza wananchi wa
mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi
32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo
Jijini Arusha waliopata ajali jana tarehe 06-May-2017 katika eneo la
Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.
Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hapo kesho.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo.

Makamu w a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo mara
baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) ambapo Mhe. Makamu wa Rais ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha
na mikoa jirani kuaga miili ya wanafunzi,na waalimu waliofariki kwenye
ajali ya gari. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...