Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetenga kiasi cha shilingi billioni mbili ili kukarabati miundombinu ya shule kongwe za Sekondari za kilakala na Mzumbe kwa wamu ya kwanza ikiwa ni kuboresha kiwango cha elimu na kurudisha umaarufu wa shule hizo ambazo zimetoa wasomi wakubwa na watalaamu mbalimbali hapa nchini.
Akiongea katika makabidhiano ya mikataba ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya shule kongwe ya Mzumbe sekondari na kilakala sekondari mkoani morogoro Kaimu mkurugenzi mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima amesema ukarabati wa shule hizo umeingia mkataba na mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya shillingi Billioni 2 kwa awamu ya kwanza huku meneja waShirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi. Veneranda Seif amehaidi kuhakikisha ujenzi wa miundo mbinu hiyo unafanyika kwa kiwango kikubwa kuhakikisha thamani ya fedha iliyotolewa inatumika kikamilifu.
Kwa upande wake mshauri wa mradi, Bw. Thomas Kalugula amesema katika upembuzi yakinifu kuna sehemu ya miundo mbinu inatakiwa kufanyiwa ukarabati ikiwemo mifumo ya maji taka katika shule hizo huku wanafunzi wakiipongeza mamlaka ya elimu Tanzania kwa kuwandalia mazingira bora ya kujisomea.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Graceana Shirima (katikati) akimuelezea mwandishi wa habari wa ITV, Bw. Sifuni Mshana (kulia) kiasi cha fedha itakayotumika katika ujenzi wa awali wa miundombinu ya shule mbili kongwe za kilakala na Mzumbe mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua kiwango cha uchakavu wa miundo mbinu hiyo.
Mshauri muelekezi wa Nousoto Associates, Bw. Thomas Kalugula akitoa taarifa ya upembuzi yakinifu wa mahitaji ya ukarabati wa shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro na kubainisha kuwa, ujenzi wa awali utahusisha mifumo ya maji taka ambayo haifanyi kazi ipasavyo huku akihaidi kuwa watasimamia ujenzi huo hadi hatua ya mwisho.
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Morogoro, Bi. Veneranda Seif akikabidhiwa mkataba wa ujenzi wa shule kongwe za Kilakala na Mzumbe ambazo zilielezwa kugharimu kiasi cha shillingi billioni mbili katika ujenzi wa awali huku mkataba huo ukimtaka mkandarasi huyo kuanza ujenzi mapema 2 Juni mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu (TEA), Bi. Graceana Shirima akiwa na timu ya wataalamu wakiwemo waandishi wa habari mkoani Morogoro katika kukagua miundo mbinu ya shule ya sekondari Kilakala ili kujionea hali halisi ya majengo na kubaini uwepo wa jengo ambalo halitumiki kutokana na kukosa ukarabati.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...