Na Dotto Mwaibale
MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.
Mwito
huo umetolewa na Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti
wa Kilimo cha Ukiliguru, Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika
mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa
na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la
Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB).
"Ni
vema kila ofisa ugani akawa na shamba la mfano ambalo litasaidia
wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo bora badala ya kuwaacha bila ya
kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya mfano.
Katika
hatua nyingine Chirimi alisema uzalishaji wa zao la pamba umeshuka
kutokana na maofisa kilimo kushindwa kuwafikia wakulima kwa ajili ya
kuwapa elimu ya kilimo bora na cha kisasa.
Alisema
kuna kila sababu ya kutolewa elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya
pamba ambayo ikitumika itaongeza tija katika uzalishaji hasa katika
kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.
Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika
mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa
na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa
hilo.
Mtaalamu
wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru
jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
Ofisa
Ushauri wa Kilimo wa Wilaya ya Buchosa, Sospeter Obwago (wa pili
kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Ofisa
Kilimo wa Wilaya hiyo, Paul Misana. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon na Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...