
Maonesho
hayo ambayo yameandaliwa na Global Education Link (GEL) kwa
kushirikiana na Ubalozi wa India nchini yatafanyika kesho katika ubalozi
huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere
(JNICC).
Akizungumzia
maonesho hayo, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel
amesema, wanafunzi wa kitanzania wamekuwa wakikumbana na changamoto
kubwa ya kudsoma katika vyuo ambavyo havina ifa.
“Unakuta
mwanafunzi anapewa taarifa ambazo si sahihi hata katika vyuo
anachokwenda, na ndio sababu tumeamua kuandaa maonesho hayo ili kubaini
vyuo sahihi,” alisema.
Amesema
wanafunzo wengi wamejikuta wakisoma katika vyuo ambavyo havina hadhi
sawa na ile waliyotegemea, hatua inayowawia vigumu katika kutambulika na
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).
Kwa
upande wake Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema maonesho hayo
yatafanyika Kesho na keshokutwa katika ubalozi wa India na kwamba lengo
kubwa ni kuwaunganisha wanafunzi wa kitanzania wanaolenga kusoma katika
nchi hiyo na vyuo vyenye ubora.
Arya
amesema maonesho hayo yatashirikisha taasisi 20 za vyuo vikuu ambazo
zinazotoa fani tofauti katika ngazi zote za elimu ya juu.
01.Mkurugenzi
wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumzia juu ya
maonesho hayo ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika
kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...