NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amewaomba wadau wamichezo
nchini kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwakuwa ni michezo kama
ilivyo michezo mingine.
Meya
Mwita aliyasema hayo jiji hapa leo katika uzindua wa mashindano ya
mchezo wa Drafti yaliyofanyika katika viwanja vya mwembe yanga,
halmashauri ya Temeke.
Mashindano
hayo ambayo yamedhaminiwa na Meya wa jiji Mwita , yalihudhuriwa pia na
Mbunge wa jimbo la Temeke Abdala Mtolea , Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo
wa Drafti ambapo jumla ya washiriki 64 walishiriki.
Meya
Mwita alisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini umekuwa ukizaraulika na
kuonekana kwamba wanaoshiriki mchezo huo niwatu ambao hawana kazi za
kufanya.
Alisema
wapo wadau wengi ambao wanatoa vipaumbele kwenye michezo ya mpira wa
miguu, mpira wa pete na michezo mingine huku wakiusahau mchezo huo ,
jambo ambalo linaonyesha kuwatenga makundi ambayo wamejikita kwenye
mchezo huo.
Alisema
“ Niwaeleze tu kwamba, huu mchezo ni mchezo mzuri kama ilivyo michezo
mingine, leo hii wanaocheza mchezo huu wanazaraulika na kuonekana kwamba
niwatu ambao hawana kazi, wasiojua kujishugulisha, jambo ambalo sio
kweli natamani mchezo huu ufahamika kama michezo mingine.
“
Kama kweli tukiunga mkono mchezo huu, ipo siku tutajenga majina yetu
kupitia mchezo huu kama ilivyokuwa kwenye mpira wa miguu, mpira wa pete,
na hata mataifa ya nje yakatuunga mkono kupitia huu mchezo” aliongeza.
Aidha
Meya Mwita katika hatua nyingine alisema kwamba ataunga mkono chama cha
mchezo huo ili waweze kukisajili na kutambulika rasmi.
Aliongeza
kuwa katika mashindano mengine , baada ya kusajiliwa kwa chama hicho,
yatakutanisha kila halmashauri iliyopo jijini hapa na hivyo kupata
mshindi kutoka kwenye halmshauri husika.
“
Jiji lina halmashauri tano, nataka kwenye mashindano mengine ambayo
tayari chama hiki kitakuwa kimesajiliwa , kila halmashauri itashiriki,
na mshindi atapatikana kutoka kwenye halmashauri nasio mmoja mmoja kama
ambavyo tumefanya leo, ila huu ni mwanzo.
Hata
hivyo Meya Mwita ameahidi katika mashindano yajayo kugharimia nauri na
chakula kwa wachezaji watakao shiriki mashindano hayo na kuwa himzi
wachezaji hao kuuthamini mchezo huo.
Awali
akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Meya wa jiji , Mwenyeiti
wa Chama cha mchezo wa huo mkoa wa Dar es salaam , Kiraba Ngibombi
amesema chama kinakabiliwa na changamo nyingi ikiwemo ukosefu wa ofisi
na fedha za kuhudumia na kufanya usajili wa chama hicho.
Mwenyekiti
huyo amemuomba Mstahiki Meya katika mashindano yajayo kuwagharimia
wachezaji chakula na pamoja na nauri kwa ajili ya wachezaji hao.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdala Mtolea akicheza mchezo wa Drafti na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...