Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compesation Fund – WCF), Masha Mshomba, (pichani) amewahamasisha waajiri nchini kujisajili katika mfuko huo kwani mkombozi mkubwa kwa waajiri na wafanyakazi.

Mshomba ametoa rai hiyo leo wakati wa siku ya wafanyakazi duniani ‘Mei Mosi” iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi mwaka huu alikuwa rais John Pombe Magufuli. 
Mfuko wa Fidia ni mkombozi kwa waajiri na wafanyakazi nchini kwa sababu umekuja katika kipindi ambacho huko nyuma tulikuwa hatuna chombo hiki,wafanyakazi walikuwa wakipata ajali na magonjwa yanayotokana na kazi bila kupata fidia sasa mfuko umekuja mambo hayo yatakuwa historia. 
 Mshomba alisema  WCF ni faraja kwa waajiri kwani utawawezesha kujikita katika uzalishaji tu, na WCF kubaki na jukumu la kumuhudumia mfanyakazi anapoumia, au kuugua. Alsema Mshomba. Alisema pamoja na kwamba waajiri ndiyo wachangiaji wakuu,mfuko wa WCF umewaondolea mzigo wa kuhangaika na mtumishi pale anapopata ajali, au maradhi yatokanayo na kazi anazofanya. 
“Tunawasihi sana waajiri waendelee kujisajili katika mfuko wa WCF kwa haraka kabisa ili waweze kunufaika wao na wafanyakazi wao,mfanyakazi akipata ajali atapata huduma ya matibabu na kama amepata ulemavu basi atapata fidia katika malipo ya pensheni ya kila mwezi”,aliongeza Mshomba.
Katika kusherehekea sherehe za Mei Mosi mwaka 2017 mfuko wa WCF umetoa elimu kwa wafanyakazi na wananchi mbalimbali waliofika katika banda lao lakini pia wafanyakazi wa WCF wameshiriki katika maandamano ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali za umma na binafsi katika viwanja vya Ushirika Moshi. Kutoka Dar es Salaam, Khalfan Said wa K-VIS BLOG anaripoti kuwa.
Wfanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wameungana na wenzao jijini Dar es salaam kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi kwa matembezi kutoka Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Uhuru.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...