Serikali
 kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi 
bilioni 63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 
tangu kuanzishwa kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za 
Mawasiliano(TTMS) nchini.
Hayo
 yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin 
Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni.
“Mtambo
 huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuongeza ufanisi 
katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi 
ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani 
kote,”aliongeza Ngonyani
“Kuanzia
 Oktoba 2013 hadi Februari 2017, kiasi cha shilingi 63,015,450,230 
zilipatika na katika hizo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina 
na shilingi bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na 
Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye 
manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya mfumo huu mapato hayo hayakuwepo.”
“Aidha
 pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili 
kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma 
za mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato 
Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea,” aliongeza Naibu 
waziri Ngonyani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...