Hospitali
ya Taifa Muhimbili-MNH- imeanza kumfanyia uchunguzi mchoraji wa Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu.
Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dk. Juma Mfinanga amesema Mzee Kanyasu amechukuliwa leo asubuhi kutoka
Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani zake na kupatiwa matibabu
ya awali.
‘’
Tumemchukua kutoka Hospitali ya Amana baada ya kupata habari zake kwenye vyombo
vya habari kuwa hali yake kiafya sio nzuri hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa MNH , Profesa Lawrence
Museru akatuagiza tumfuate ili apatiwe matibabu hapa Muhimbili ‘’ Amesema Dk.
Juma.
‘’
Wenzetu wa Hospitali ya Amana wamemfanyia uchunguzi wa awali na wakatueleza
shida yake kubwa ni kukosa nguvu na kushindwa kutembea hivyo tumemleta hapa Idara
ya magonjwa ya Dharura na Ajali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Baada ya uchunguzi tutamuanzishia tiba haraka kwa kushirikiana na Idara zingine hapahapa
MNH.’’ Amesema Dk. Juma.
Kwa
mujibu wa Dk. Juma kukosa lishe ,
mazingira magumu pamoja na umri kunasababisha mtu kupata magonjwa mbalimbali.
Mchoraji Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu akiwa
katika Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
ajili ya uchunguzi wa afya yake. Mzee Kanyasu amefikishwa leo MNH akitokea
Hospitali ya Amana.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni Mkuu wa Idara hiyo
Juma Mfinanga akimuhudumia Mzee Kanyasu mara baada ya kufikishwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...