Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Biashara litakalofanyika kesho May 11 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika Kongamano hilo, Mhe. Zuma ataongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, pamoja na Wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari amesema kuwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia kituo hicho wameandaa Kongamano hilo, na kutoa wito kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kukutana na Wafanyabiashara wenzao wa nchi hiyo ya Afrika Kusini.

Tandari amesema kuwa Sekta kubwa zitakazojadiliwa katika Kongamano hilo ni Sekta ya Nishati, Viwanda, Miundombinu, Uchukuzi, Usafirishaji, Huduma ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Maji na Madini.

Pia amesema Afrika Kusini ni Taifa ambalo lipo katika nchi kumi bora zilizowekeza kwa wingi hapa nchini, hivyo ni fursa kuchamshana kiuchumi, pia wameandikisha miradi 63 ambayo imeajiri vijana wengi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu Kongamano la Biashara litakalofanyika May 11 mwaka huu jijini Dar na kuhudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...