Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Serikali ya Mkoa wa Tabora imewaagiza kwa wakazi wa Mkoa huo kuanza kulima kwa wingi mazao wengine kama vile alizeti , pamba,  mpunga na miembe ya kisasa ili waweze kuwa na fursa pana ya kujiongezea kipato badala ya kutegemea tumbakuli pekee kama zao kuu la uchumi katika maeneo mengi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati anawahutubia wakazi na Wafanyakazi kwenye sherehe za kilele cha Mei Mosi kilichofanyika katika Maspiaa ya Tabora.

Alisema kuwa Mkoa huo umebahatika kuwa na ardhi ambayo mazao mbalimbali kama vile mpunga , pamba, alizeti na hata matunda kama vile maembeo yanastawi , lakani bado wananchi hawayapa kipaumbele.

Bw. Alisema kuwa wananchi wakiyapa kipaumbele na kwa kuzingatia ukulima wa kisasa yatasaidia kufungua fursa ya uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo kuelelekea viwanda vikubwa kwa kuwa malighafi itakuwepo ya kutosha viwanda vitakavyoanzishwa.

Aliseme kuwa endapo kila familia itakuwa walau na hekari moja ya shamba la alizeti Mkoa wa Tabora utakuwa ndio mzalishaji mkubwa na mafuta hayo na wawekezaji wengi watajitokeza kuanzisha viwanda wa usindikaji wa zao hilo na hivyo kutoa ajira kwa wakazi wengi na wakinamama kupata fursa ya kuuza vyakula.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa Tabora inayofursa kubwa ya kuwa na viwanda vikubwa vya kusaga na kukoboa nafaka endapo wakulima watalima mpunga na mahindi kwa wingi na kwa kuzingatia utaalam.

Kuhusu suala la kilimo cha miembe, mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa wakazi wa kuanza kuwa na mashamba makubwa ya miembe ya kisasa kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa matunda hayo kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani.

Alisema kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora imeshaanza taratibu mbalimbali za kuhakikisha kuwa viwanda vya zamani vinafufuliwa na vipya kama vile vya kusindika tumbaku vinajengwa ili kuongeza ajira kwa wakazi wa Tabora.

Aidha alitoa kwa wafanyakazi wote Mkoani humo kuonyesha mfano kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kilimo kwa kuwa na mashamba ya kisasa kama sehemu ya kuhamasisha wananchi juu ya kilimo cha kisasa ambacho kinafaida zaidi.

Maadhimisho ya Mei Mosi Kimkoa yamefanyika katika Manispaa ya Tabora ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki , Masilahi na Hershima ya Wafanyakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...