Bi. Vicky Joan Msina wa Benki Kuu
Dar es Salaam, kwa niaba ya ndugu zake wote na familia za Msina, Lyimo, Kiiza
na Mbuya wa Dar es Salaam, Kilema, Moshi, na Tabora; wanapenda kutoa shukrani za
dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kipindi chote cha kumuuguza
na kushiriki shughuli ya msiba wa Mama yao mpendwa Mwalimu Petronella Peter
Lyimo, aliyefariki Ijumaa tarehe
28 Aprili, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na
kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele tarehe 04 Mei, 2017
Mbweni, Dar es Salaam.
Shukran za
pekee ziwafikie Madaktari na Wauuguzi wa Hopitali ya St. Joseph- Mbweni, Rabininsia
na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili za Dar es Salaam.
Pia Shukran ziwafikie
Majirani wote wa Mbweni wakiongozwa na Bwana na Bibi Mutegeki, Bi Sandra na
wengine wote, pamoja na Wana Jumuiya ya mtakatifu Joseph Mfanyakazi – Mbweni
kwa kutufariji kwa hali na mali. Vile vile shukran ziende kwa Baba Paroko, Paroko
msaidizi na Katekista na wanakwaya wa Parokia ya Mtakatifu Rafael - Mbweni kwa
huduma ya kiroho waliyotoa kwa marehemu wakati wa uhai wake na pia kwa
kufanikisha Ibada ya Maziko kwa kushirikiana na kaka wa Marehemu Fr. Henry
Zawadi wa Kristo Mfalme Moshi.
Kwa namna ya
kipekee tunawashukuru sana Uongozi na Wafanyakazi wa Benki Kuu Tanzania, Wizara
ya Fedha na Mipango, NMB- Makao Makuu na Tawi la Bank House, Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Shule ya Msingi za Pwani-
Tegeta na Kiumbageni-Mbweni pamoja na Shule maalum ya wasiosikia- Njombe.
Ni ngumu
kumtaja kila mmoja kwa namna mlivyoshiriki kutufariji katika kipindi hiki
kigumu. Tunasema kwenu nyote Asanteni sana na Mungu awabariki daima.
PUMZIKA KWA
AMANI MAMA YETU MPENDWA Mwl. PETRONELLA LYIMO.
“BWANA AMETOA
NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...