Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameondoka
nchini leo kwenda Kigali Rwanda, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye mkutano wa
siku mbili wa “Transform Africa Summit 2017”.
Mkutano huo utawakutanisha viongozi na wataalam mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kujadili masuala kadhaa ikiwemo maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), hususan katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika mkutano huo, Profesa Mbarawa ataeleza kwa kina changamoto na mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika uwekezaji wa Miundombinu ya Habari na Mawasiliano, Maendeleo ya Sera na Miongozo inayotumika hapa nchini katika kusimamia sekta hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuiunganisha Tanzania na Mataifa mengine.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
10 Mei, 2017

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...