NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.

BENKI ya DTB kwa kushirikiana na EFM Radio kupitia kipindi chake cha “Bustani ya Watoto”, wametoa msada wa madawa mbalimbali kwa Taasisi ya Mifupa MOT iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo Juni 18, 2017.

Akikabidhi madawa hayo, Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Bi.Jesca Mwanyika alisema, EFM kupitia kipindi chake cha watoto cha “Bustani ya Watoto” iliamua kuwashirikisha DTB ili kuona ni namna gani wanaweza kusaidia watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya MOI hususan wale wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.

“Sisi kama EFM Radio tuna kipindi cha watoto cha Bustani ya Watoto, tumeona kwa vile tunashughulika na watoto, na kwa vile siku chache zilizopita Dunia iliadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Duniani, basi tumeona tutoe kiasi hiki cha madawa kuwasaidia watoto hawa wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa hapa MOI.”Alisema Bi. Jesca.

Akizungumza kwa niaba ya DTB, Afisa Masoko wa benki hiyo, Bw.Baguma Ambari alisema, Benki kama taasisi inayotoa huduma kwa wananchi, inao wajibu mkubwa kutoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii na hivyo imefurahishwa kuungana na EFM Radio katika kutoa msada huo wa madawa ambao anaamini utasaidia katika kuwahudumia watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt.Respicious Boniface, (kulia), akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Meneja wa Benki ya DTB Tawi la Morocco jengo la Airtel, jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena .Y. Sinare, kwenye jengo jipya la MOI, leo Juni 18, 2017. DTB kwa kushirikiana na EFM Radio, wametoa msada wa madawa mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Dkt. Boniface, akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika kwenye jengo jipya la MOI jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2017. EFM kwa kushirikiana na Benki ya DTB wametoa msada huo wa madawa yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matataizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI, akikabidhi sehemu ya msada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Precious Boniface

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...