Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha
Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
wilaya katika ziara yake juzi.
Meneja
Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo,
Andrew Hooper (katikati) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa
maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai namna mitambo ya
kuchakata Gesi inavyofanya kazi wakati wa ziara yao walipotembelea
chumba maalumu (Control room) katika mitambo ya Gesi Songas iliyopo
katika kisiwa hicho juzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...