KIJANA Abdulmjid
Mujahid kutoka Yemen ameibuka mshindi wa mashindano ya kimataifa ya
Qur-an yaliyozishindanisha nchi kumi ambapo mshindi amezawadiwa dola
5000 za kimarekani huku ubalozi wa Kuwait ukimzawadia dola 500, mshindi
wa pili wa mashindano hayo ni Omary Abdallah kutoka Tanzania ambaye nae
amezawadiwa dola 4000 na dola 300 kutoka ubalozi wa Kuwait.
Mashindano hayo yameshirikisha nchi kumi zikiwemo Uganda, Mali, Tanzania Bara, Yemen, Russia, Uingereza, Libya, Bangladesh, Marekani na Jumuiya ya Falme za kiarabu (United Arab Emirates).
Mashindano hayo yameshirikisha nchi kumi zikiwemo Uganda, Mali, Tanzania Bara, Yemen, Russia, Uingereza, Libya, Bangladesh, Marekani na Jumuiya ya Falme za kiarabu (United Arab Emirates).
Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya
dola za Kimareni 5,000 mshindi kwanza wa mashindano ya kimataifa ya
Qur-an Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen leo jijini Dar es Salaam.
Pia
Mashindano hayo yameudhuriwa na viongozi mbalimbali yakiongozwa na
makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy, na mlezi wa Jumuiya ya
Kuhifadhisha Qur-an Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, Muft Mkuu wa
Tanzania Abubakar Zuber, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad
Mussa Salum, mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na mgeni
maalum kutoka Saudi Arabia Abdallah Basfar ambaye ni msomaji Qur-an wa
kimataifa.
Akihutubia katika mashindano hayo Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Ally Seif Iddy ameeleza kuwa vijana wamekosa adabu na matendo ya ulawiti, mauaji kwa watoto wachanga, unyanyasaji, mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiripotiwa, huku akieleza kuwa aamini kama Mwenyezi Mungu anayaridhia matendo haya, hivyo tabia za watanzania na waislamu ziendane na maamrisho ya Qur-an.
Akihutubia katika mashindano hayo Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Ally Seif Iddy ameeleza kuwa vijana wamekosa adabu na matendo ya ulawiti, mauaji kwa watoto wachanga, unyanyasaji, mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiripotiwa, huku akieleza kuwa aamini kama Mwenyezi Mungu anayaridhia matendo haya, hivyo tabia za watanzania na waislamu ziendane na maamrisho ya Qur-an.
Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya
dola za Kimareni 4,000 mshindi pili wa mashindano ya kimataifa ya
Qur-an wa Tanzania,Omary Abdallah leo jijini Dar es Salaam.
Pia
Makamu wa Rais Balozi Seif Ally Iddy ameongeza kuwa mbora ni mwenye
kujifunza Qur-an na akawafundisha wengine Mwenyezi Mungu amewanasihi
waislamu katika kitabu chake kitukufu.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi awapongeza wanafunzi wa kiislamu wanaojifunza Qur-an kwani kufanya hivyo ni kuiendea jamii njema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amewataka wadau wa masuala ya Qur-an kuhakikisha Qur-an inakaa katika nyoyo za vijana ili jamii iweze kuwa bora na kuheshimiana wakubwa kwa wadogo.

Rais
Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akipokea tuzo ya
heshima kutoka Muft wa Tanzania Abubakar Zuber iliyotolewa na Jumuiya ya
kuhifadhisha Qur-an Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya kusoma
Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam leo.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA, GLOBU YA JAMII.
Huku Muft Mkuu wa Tanzania Abubakari amesema ni vyema watu wakajifunza Qur-an kwasababu ni dawa ya kila tatizo, endapo waja wataifuata kwa mafunzo yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa, kwani Qur-an imekataza kuuana, kuchukiana, kuvuruga amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...