MOTO wa bahati nasibu ya Biko ama ‘Ijue Nguvu ya Buku’,
umezidi kuchanja mbuga baada ya droo yake ya 14 kufanyika leo jijini Dar es
Salaam, huku mkazi wa Kilosa Morogoro, Magreth Sinyangwa, akiwa mwanamke wa
kwanza kuzoa jumla ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa bahati
nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini.
Droo hiyo iliyompelekea utajiri mshindi huyo wa Morogoro,
imechezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja na kushuhudiwa pia na
mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa droo hiyo, Meneja
Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema moto wa Biko umezidi kuchanja mbuga
baada ya kumpata mshindi wao wa Sh Milioni 20, huku kwa mara ya kwanza
wakimpata mshindi ambaye ni mwanamke tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu yao.
Alisema washindi hao ni wale wanaocheza bahati nasibu yao kwa
njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za
M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money, ambapo watatakiwa kuingia kwenye lipa bili
au lipa kwa M-Pesa na kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na namba ya
kumbukumbu 2456 tayari kwa kucheza.
“Baada ya kuingiza namba ya kumbukumbu pia atatakiwa kuweka
kiasi cha kucheza ambacho kinaanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo kiasi cha Sh
1000 kitampatia nafasi mbili ambazo ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na donge
nono la Sh Milioni 20 kwa Jumapili ijayo kama tulivyompata mwingine kwa droo
tuliyochezesha jana.
“Kwa zawadi za papo kwa hapo zinaanzia Sh 5000, 10,000,
20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambapo mshindi hutumiwa
fedha zake dakika chache baada ya kupokea ujumbe wa Biko ukimtaarifu juu ya
ushindi wake kutokana na kucheza Bahati Nasibu yetu,” Alisema Heaven na
kuwataka Watanzania wacheze mara nyingi zaidi ili waweze kujiwekea mazingira
mazuri ya kuibuka na zawadi mbalimbali za Biko.
Balozi wa Biko Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, wakihakiki namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Sinyangwa na kumpigia ili kumjulisha juu ya ushindi wake.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akiagana na mwakilishi wa Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, mara baada ya kumaliza kuchezesha droo ya 14 ya Sh Milioni 20 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam, huku Magreth Sinyangwa akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na mamilioni hayo ya Biko tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu hiyo hususan kwa droo kubwa za Sh Milioni 10 hadi 20.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...