Naibu Mhifadhi (Huduma za Shirika) wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye N. Bangu (kushoto), akipeana mkono na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa TFF wa Maendeleo ya Soka (TFDF), Derek Murusuri. Bw Bangu alizitembelea ofisi za TFDF ili kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mamlaka yake na Mfuko huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za TFDF zilizoko Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo (28 June 2017).
Katika mazungumzo hayo, Bw Bangu ameahidi kushirikiana na Mfuko huo katika kuendeleza soka la Tanzania.
Timu ya Taifa ya vijana walio chini ya miaka 20 (U-20), Ngorongoro Heroes, inatumia jina la Mamlaka hiyo ya Taifa ambayo pia ni mojawapo ya maajabu saba ya dunia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...