Mkuu wa Itifaki mstaafu Marehemu Balozi Abdul Omar Cisco Mtiro (pichani) ambaye alifariki dunia jana asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa kesho JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo.
 Bw. Mtambo ameiambia Globu ya Jamii kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo nguli yamepangwa kufanyika kesho saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
"Hiyo ni baada ya kuwasili watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili Jumanne usiku, pamoja na mjane wa marehemu anayetegemewa kuwasili leo mchana akitokea Bangui, Afrika ya Kati", amesema Bw. Mtambo.
Amesema ratiba ya siku ni kwamba mwili unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya JUMATANO ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.
 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole kutwa nzima ya leo.
Mapema jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un 
( إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ‎‎)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...