Tanga, SERIKALI imeshauriwa kuweka kanuni ya majengo ya gorofa na taasisi za huduma za kijamiii kujenga miundombinu maalumu kwa walemavu lengo ikiwa ni kuzifikia huduma kama ilivyo kwa wengine.
Wakizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Kituo cha Watoto Walemavu (YDPC), na kuishauri kutoruhusu ujenzi wa majengo ya huduma za kijamii bila kuwepo kwa miundombinu ya walemavu.
Imesemwa kuwa majengo mengi ya huduma za kijamii hayana miundombinu kwa walemavu hivyo kunyimwa fursa ya kupata huduma kama ilivyo kwa wengine. Imesemwa katika kongamano hilo, kuwa kutokuwepo kwa sheria watu wengi hujenga majengo bila kuweka miundombinu ya walemavu.
Imesemwa kuna baadhi ya walemavu wa viungo wenye elimu hupoteza nafasi ya kazi kutokana na majengo wanayopangiwa kazi kutokuwa na njia maalumu kwa walemavu wa viungo na kuwa kero kwao.
Mwanafunzi mlemavu kituo cha Watoto wenye Ulemavu wa viungo na ngozi, Imamu Amir, akipanda mbegu ya muhongo katika shamba la kituo hicho kijiji cha Mleni Amboni Tanga, ujumbe huo pia ulitembelea katika shamba hilo ambalo watoto walemavu wamekuwa wakiendesha kilimo cha chakula na mbogamboga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...