Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
Kamishana
wa usimamizi wa mipaka idara ya Uhamiaji Tanzania, Samwel Magweiga,
amepiga marufuku Mawakala wanaojihusisha na shughuli za uhamiaji na
kuwataka waache mara moja kufanya hivyo.
Badala yake amewataka wananchi wanaohitaji huduma hiyo kufika ofisi husika ya Uhamiaji.
Kamishana
Magweiga ametoa wito huo leo, wakati akizungumzia ukamatwaji wa watu watano wenye umri wa kati ya miaka 55 na 64 ambao walikutwa
wakimiliki ofisi na mitambo wa kughushi nyaraka mbalimbali ikiwamo ya
kughushi miradi ya maendeleo ya Serikali na machine za risiti za
kielektroniki (EFDs).
Kufuatia ukamataji huo, Kamishna
Magweiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa idara ya Uhamiaji ili
kudhibiti mianya ya watu wanaojihusisha na kughushi nyaraka za aina
mbalimbali kwa kuwa zinapelekea uhujumu wa uchumi.
Mapema
wiki hii, makachero kutoka ofisi za uhamiaji baada ya kupata taarifa
kutoka kwa wasalimia wema kuhusu kuwepo kwa hujuma hiyo, walifanya msako
na kuwakamata wazee watano ambao ofisi yao ipo eneo la BibiTiti
Mohammed kiwanja namba 16/47 lililopo Wilaya ya Ilala mtaa wa Mtendeni.
Wazee
waliokamatwa ni Hemed Ali Mchepe(56), Edga Samson Mwafongo(55), Huruma
Mwakidete(57), David Tumpange (64),At human Mohammed (61) na Simon
Joseph Veso (62).
Amesema, “kuna magenge ya wahalifu
huko mitaani ambao wanafanya kazi kwa niaba ya serikali, hawa ni
wahujumu uchumi, ni lazima wafichuliwe.” Amesisitiza Kamishna Magweiga.
Ameongeza
kuwa, nyaraka hizo za mara nyingi zimekuwa zinatumika kuchukua hati za
kusafiria, mikopo benki na kupelekea benki husika kupata hasara na
serikali kukosa mapato.
Amesema, upelelezi dhidi ya
watuhumiwa hao umekamilika na siku yoyote watapelekwa mahakamani ila
badoa wanahitaji kujua mtandao wao ni mkubwa kiasi gani na upo hapa
nchini pekee ama na nje ya nchi.
Wakielezea jinsi
walivyokamatwa mbele ya Kamishana mzee David Tumpange alikubali kuwa
yeye ni mmiliki wa ofisi iliyokutwa na nyaraka hizo za kughushi iliyopo
eneo la barabara ya Bibi Titi Mohammed na kwamba yeye hashughuliki nayo
alimkabidhi ndugu yake Huruma Mwakidete.
Aliongeza
kuwa, kwa sasa yeye anajishughulisha na masuala ya ujenzi na siku ya
tukio, alikwenda kwenye ofisi yake hiyo kwa ajili ya kumsalimia ndugu
yake huyo aliyemkabidhi ofisi na vyote vilivyokutwa humo havitambui.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...