Benki ya Ecobank Tanzania leo imeingia katika ushirikiano rasmi na TICTS, ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank. 

Benki hii imeanzisha mfumo ambao utawawezesha wateja wa TICTS kufanya malipo yao papo kwa hapo kupititia mfumo huu rahisi. Huduma hiyo itakuwa inapatikana kwa wateja wa Ecobank na wasio wateja wa benki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank, Raphael Benedict alisema benki hiyo inataka kuhakikisha huduma ya uagizaji na utoaji mizigo bandarini katika Bandari ya Dar es Salaam inakuwa rahisi zaidi na ya haraka zaidi kwa wateja wa TICTS.

Benedict aliongeza kuwa ili kuwezesha jambo hilo, Ecobank Tawi la PSPF ambalo linapatikana karibu na geti la ofisi za TICTS, limeogeza muda wa huduma zake na sasa litakuwa likifunguliwa saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia)  akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na TICTS ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini ambapo katika kufanikisha jambo hilo benki imefungua Tawi lake katika jengo la PSPF linalopakana na geti la ofisi za TICTS, huku muda wa huduma ukiongezwa kuanzia saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe wakisaini mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakipeana mkono baada ya kutia saini ya mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia (kulia) ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa fedha wa Ecobank Africa, Isaac Kamuta, Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai (wa pili kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa (kushoto). 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakibadilisha mikataba ya makubaliano ya kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mikataba hiyo ilisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...